14 Februari 2022 - 14:21
Borell: Hatutafunga ofisi yetu ya diplomasia huko Ukraine

Mkuu wa Sera za Kigeni wa Umoja wa Ulaya amesema kuwa umoja huo hautafunga ofisi yake ya diplomasia huko Ukraine. Hiyo ni kufuatia Marekani kudai kuwa upo uwezekano wakati wowote kuanzia sasa wanajeshi wa Russia wakaanzisha mashambulizi dhdi ya Kiev.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Licha ya Russia kutangaza kuwa haina nia ya kuishambulia Ukraine, Marekani na waitifaki wake wanaendelea kutoa madai mbalimbali lengo likiwa ni kuchochea moto wa vita huko Ukraine. Baadhi ya nchi tayari zimewatolea wito raia wao kuondoka Kiev kufuatia propaganda hizo za Marekani na waitifaki wake. 

Josep Borell amebainisha kuwa: Umoja wa Ulaya na nchi wanachama wa umoja huo tayari zimeratibu hatua zao kwa ajili ya kukabiliana na vitisho vilivyopo huko Ukraine. Taarifa ya Mkuu wa Sera za Kigeni wa Umoja wa Ulaya imeongeza kuwa, ofisi ya uwakilishi wetu huko Ukraine haitafungwa, wawakilishi wetu watabaki huko Kiev na wataendelea kufanya shughuli zao za kuwalinda raia wa Umoja wa Ulaya kwa kushirikiana na viongozi wa Ukraine.  

Josep Borell amebainisha kuwa, tunasisitiza tena kwamba hujuma yoyote ya kisiasa dhidi ya Ukraine itakuwa na taathira kuu na  gharama kubwa. Uhusiano wa Marekani, Magharibi na Russia uliathiriwa na mivutano tokea mwaka 2014 baada ya kisiwa cha Crimea kujiunga na Russia. Aidha nchi za Magharibi zimeiwekea Russia vikwazo mara kadhaa kwa kisingizio kwamba Moscow inaingilia masuala ya ndani ya Ukraine; madai ambayo yamekanushwa na Moscow.  

342/